Mafuriko nchini Libya yaliyosababishwa na kimbunga Daniel yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 2,000 na maelfu kutoweka, mkurugenzi mkuu anayesimamia mashariki mwa nchi hiyo amesema siku ya Jumatatu.
“Idadi ya watu ambao hawajulikani waliko inahesabilika kwa maelfu na waliofariki ni zaidi ya 2,000,” amesema Osama Hamad katika mahojiano kwa njia ya simu na kituo cha televisheni cha nchini humo cha Al Massar. Hakutaja ni wapi alitoa idadi hii , ambayo inaweza kuongezeka kwa saa zijazo.
Kimbuka kikali kutoka Mediterranean, Daniel, ambacho kilipiga mashariki mwa Libya siku ya Jumapili na Jumatatu, kilisababisha mafuriko
na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyumba na mali kadhaa. Mamlaka ina hofu kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka.
“Takriban watu zaidi ya 2,000 wamefariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Daniel huko Derna, maeneo ya Jabal Al-Akhdar na vitongoji vya Al-Marj,” Mohamed Massoud, msemaji, wa serikali iliyoko mashariki ameliambia shirika la habari la AFP. (mashariki).
Kimbunga Daniel, pia kilipiga Ugiriki, Uturuki na Bulgaria, na kuua watu wasiopungua 27.