Habari za Mastaa

Kesi ya Lil Wayne na Birdman vipi? Ni kweli Birdman hakuhusika kabisa..?

on

brdman1

Ni mwezi mmoja umepita toka Lil Wayne na Birdman waziandike headlines baada ya ugomvi wao kuwa mkubwa kufikia Birdman kulipiga risasi Tour bus la Lil Wayne ili kumuua.

Polisi wanasema Birdman na rappa Young Thug walipanga na kushirikiana kisiri kumua Lil Wayne, Birdman aliamua kumpigia simu Lil Wayne na kumwambia kuwa yeye hakuhusika kwa njia yoyote ile kwenye tukio hilo.

birdman2

Tetesi nyingi zilizosambaa ni kwamba Birdman alipokea simu kutoka kwa Young Thug na Jimmy Winfrey baada ya tukio hilo kutokea April 26 Atlanta lakini ripoti zinasema kwamba mtu kutoka kwenye kundi la Lil Wayne alimpigia simu Birdman kumtaarifu kuhusu tukio hilo.

Kuwapata watu waliohusika moja kwa moja imekuwa ngumu kwasababu ripoti zinasema kwa simu zote zilizopigwa zilikuwa chini ya jina la Birdman na zinalipiwa na Cash Money Records. Birdman bado anasema hakuhusika na tukio hilo.

birdman4

Jimmy Winfrey alikamatwa na polisi dhidi ya makosa tofauti baadhi yakiwa kosa la shambulio la mwili, kauli za kigaidi na kukamatwa na silaha kali ikiwemo visu na bunduki, amekataliwa dhamana na sasa yupo jela anasubiria tarehe yake ya kwenda Mahakamani.

 Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments