Habari za Mastaa

Kwa nini nyimbo nyingi za Drake ni za mapenzi na wanawake…?! Lil Wayne atoa hizi sababu.

on

Rapper maarufu kutokea kwenye kundi la Cash Money Records Lil Wayne ndiye aliyehusika kwa asilimia kubwa sana kikigundua kipaji cha rapper Drake na kumleta kwenye lebo yake ya Young Money Music.

Hivi karibuni Lil Wayne alialikwa kwenye kipindi cha Tv kiitwacho Be Honest podcast with ESPN’s Cari Champion na akiwa kwenye kipindi hicho Lil Wayne alisikika akisimulia kitu gani alichomueleza Drake kabla ya kumuweka chini ya lebo yake…

weezy1

>>> “Mimi ndiye niliyekuwa nikimwambia kuwa, “usibadilishe chochote”… nilisisitiza sana aimbe rap anayoiweza zaidi, rap ya mambo ya mapenzi kwa sababu gani nilimwambia hivyo, Drake anauwezo mkubwa sana wa kutunga mashairi ya kuimba na rap ya kimapenzi ambayo yanagusa wengi… nilimwambia pia “kwa sababu tu unakuja kuwa chini yangu na kwenye lebo yangu haimanishi na wewe uimbe kama navyoimba mimi.. kuwa original, kuwa wewe, kuwa Drake na sio Lil Wayne”. <<< Lil Wayne.

Kabla ya Drake kuwa rapper alionekana kwenye kipindi cha MTV kiitwacho Degrassi na alipoaanza kurap, alirap kuhusu mapenzi na wanawake…

weezy2

>>> “Nilimsisitiza Drake aimbe rap inayowahusu wanawake, kwasababu nyota yake imelala kwenye mashairi ya namna hiyo na sio muziki kama ninaoufanya mimi. Nilimwambia asiimbe kuhusu mambo ya kitaa. Nilimwambia kuwa wewe, unawapenda sana wanawake so rap kuhusu wao!”<<< Lil Wayne.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments