Michezo

Lionel Messi ashinda tuzo ya 6 ya Ballon d’Or na kumuacha Ronaldo

on

Usiku wa December 2019 nchini Ufaransa katika jiji la Paris zilifanyika tuzo za Ballon d’Or 2019, huku wengi wakitaka kujua ni nani atakuwa mshindi kati ya Van Dijk, Ronaldo na Lionel Messi.

Lionel Messi wa FC Barcelona ndio mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or 2019, hiyo ikiwa ni tuzo yake ya 6 ya Ballon d’Or akimzidi mpinzani wake wa muda wote Cristiano Ronaldo aliyewahi kutwaa tuzo hiyo mara 5.

Wengine waliofanikiwa kushinda tuzo katika usiku wa Ballon d’Or 2019 ni beki wa Juventus Matthijs De Light tuzo ya mchezaji bora kijana (Kopa Trophy) kwa kuwashinda Jadon na Joao.

Golikipa wa Liverpool Alisson Becker akiwa ndio mshindi wa tuzo ya kipa bora wa mwaka na Megan Rapinoe wa timu ya taifa ya wanawake ndio akashinda tuzo ya mchezaji bora wa kike (Ballon d’Or).

Soma na hizi

Tupia Comments