Michezo

Lionel Messi amenusurika Mahakamani, baba yake ataikwepa miezi 18 jela?

on

Unaikumbuka ile kesi ya Lionel Messi na baba yake mzazi Jorge Messi kutuhumiwa kukwepa kodi? basi stori kutoka mtandao wa the42.ie kuhusu muendelezo wa kesi hiyo unaeleza kuwa waendesha mashitaka nchini Hispania wameona Lionel Messi hana Kesi ya kujibu ila baba yake anayo kesi ya kujibu.

Lionel-Messi-goals-Season-201516

Ripoti kutoka mtandao huo unaeleza kuwa waendesha mashitaka wa Catalunya wameona Lionel Messi hana kesi ya kujibu ila baba yake Jorge Messi itamlazimu kutumikia kifungo cha miezi 18 jela kama akikutwa na hatia ya kosa la ukwepaji kodi. Lionel Messi na baba yake walikuwa wakituhumiwa kukwepa kulipa kodi kiasi cha euro milioni 4.1 kati ya mwaka 2007 hadi 2009.

Lionel-Messi-Jorge-Messi

Lionel Messi na baba yake Jorge Messi

Jorge Messi ambaye ni baba wa Lionel Messi anatuhumiwa kwa kosa la ukwepaji kodi, kwani yeye ndio muhusika mkuu wa tukio hilo ambaye huwa anasimama kama wakala wa Lionel Messi katika shughuli zake mbalimbali.

Lionel Messi kwa sasa yupo nje ya uwanja kwa muda wa wiki nane akiuguza jeraha lake.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments