Top Stories

Prof. Lipumba kafanya maamuzi magumu, tujikumbushe pichaz UKAWA walivyompokea Lowassa…

on

3X6A9441

Hapa ilikuwa meza kuu, yuko Freeman Mbowe (CHADEMA), Edward Lowassa (CHADEMA) na Prof. Lipumba (CUF)

Ulimwengu wa Siasa Tanzania August 06 2015 umepokea headlines nyingine zenye uzito ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho.

Kwenye kile alichokisema wakati anatangaza kujiuzulu, yako na maneno mengine haya hapa >>> ‘Ni kweli nilishiriki kumkaribisha Lowassa UKAWA lakini dhamira na nafsi yangu inanisuta… Tumekaribisha watu wa CCM ambao waliipinga Rasimu ya Katiba, najiuliza tutaweza kusimamia malengo ya UKAWA‘ >>>> Prof. Lipumba.

Zari

Sentensi nyingine amesema hivi >>> ‘Taarifa ya kung’atuka niliitoa August 01 2015, nilisubiri kukamilisha masuala ya UKAWA ndio nitoke… Ninaendelea kuwa Mwanachama wa CUF na nimelipia Kadi ya Uanachama mpaka 2020, sina mpango wa Kujiunga ACT‘- Prof. Lipumba.

Hapa nina pichaz nyingine Kumbukumbu ya July 28 2015 siku Edward Lowassa alivyokaribishwa rasmi CHADEMA na UKAWA.

3X6A9526

Lowassa na Mama Regina Lowassa wanakumbatiana, pembeni yao ni Prof. Lipumba.

3X6A9531

Edward Lowassa na Prof. Lipumba walikuwa wamekaa karibu kwenye meza kuu muda wote.

3X6A9628

Edward Lowassa na Prof. Lipumba kuna wakati walikumbatiana.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments