Top Stories

Lisa mwanamke wa kwanza kunyongwa Marekani toka 1953

on

Lisa Montgomery ameingia kwenye rekodi za kuwa Mwanamke wa kwanza kunyongwa Nchini Marekani toka mwaka 1953, yani kwa karibu miaka 70 Marekani haijawahi kunyonga Mfungwa Mwanamke.

Lisa amenyongwa kwa kuchomwa sindano ya sumu kwenye gereza la Terre Haute huko Indiana ambapo kabla ya kuchomwa sindano hiyo aliulizwa kama kuna kitu cha mwisho angependa kusema au kuongea ambapo alijibu hamna.

Lisa alihukumiwa kifo mwaka 2008 baada ya kufanya mauaji ya Mwanamke Mjamzito mwaka 2004 aitwae Bobbi ambapo inadaiwa siku ya tukio alikwenda kwa Mwanamke huyo kwa lengo la kununua Mbwa lakini akaishia kumnyonga na kumkata tumbo na kuchukua Mtoto aliyekua ndani.

Pamoja na kwamba Mawakili wake waliwasilisha utetezi kwamba Lisa amekua na tatizo la akili toka Mdogo, utetezi huo haukuzuia kutekelezwa kwa hukumu hiyo ya kifo kwa Lisa.

MAGUFULI AMUACHA HOI MCHINA “HAJAVAA BARAKOA SABABU HATUNA CORONA, NAMSHIKA MKONO”

Soma na hizi

Tupia Comments