Baada ya Serikali kukusudia kupeleka Bungeni muswada wa Sheria utakaofuta Sheria iliyoianzisha TLS mwaka 1954 ikiwa ni pamoja na kutengenisha shughuli za Uwakili na Chama hicho, Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema hatua hiyo inakusudia kubadilisha muelekeo wa taaluma ya Sheria na kuminya Uhuru wa Mawakili kuwatetea Wananchi.
Tundu Lissu alisema:>>>Baada ya kuletewa na Wizara ya Katiba na Sheria kitu wanachokiita Bango Kitita chenye mapendekezo ya kufanyia marekebisho makubwa katika utaratibu mzima wa Taaluma ya Sheria katika Tanzania. Mapendekezo ambayo tumeletewa ni makubwa kwa sababu yataleta mabadiliko makubwa sana katika mfumo mzima wa Taaluma ya Sheria.
“Tumekuwa na Chama cha Mawakili wa Tanganyika ambacho kinashughulikia masuala yote yanayohusu maslahi ya Mawakili pamoja na masuala yanayohusu Utawala wa Sheria. Mawakili na Chama chao kwa mfumo wa kisheria na Katiba wa kwetu ni sehemu kamili ya mfumo wa utendaji Haki.
“Ili Mawakili waweze kusaidia watu kupata Haki zao wasiingiliwe katika masuala yao ya kitaaluma. Waweze kusaidia jamii kupata Haki bila ya wao kuwa na hofu kwamba mambo yao, maslahi yao, Haki zao zitaathiriwa. Ndiyo maana ya kuwa na Chama huru cha Mawakili na kuwa na utaratibu Huru wa kisheria unaohakikisha kwamba Serikali haiingilii mambo ya Mawakili.” – Tundu Lissu.
MAAJABU?!! TUMBO LIMETOBOLEWA LAKINI ANATEMBEA!!!