Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara Tundu Lissu leo katika mkutano wa Chama hicho Jijini Arusha, amesema kama katika kipindi hiki cha uhaba wa sukari Serikali inaagiza sukari kutoka nje na kuiingiza Nchini bila kuitoza kodi ‘duty free’, ni kwanini iuzwe elfu tano au elfu sita kwa kilo ?
Kwa upande mwingine, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara Tundu Lissu ameoneshwa kutopendezwa na kitendo cha Polisi kuwataka Waandamanaji wapite kwenye upande mmoja wa barabara ili kuruhusu magari yapite upande mwingine.
“Wanatuambia Waandamanaji lazima muandamane upande mmoja ili magari yapite, maandamano yenu yasizuie magari………. Mwanza, Mbeya, Dar es salaam ilikua hivyohivyo, sasa Ndugu zangu Dunia nzima kazi ya kwanza wanayofanya Mapolisi ni kusafisha njia, ni kuondoa magari barabarani, Polisi fanyeni kazi yenu ya kutusaidia kuandamana kama mnavyomsaidia Makonda” ——— Tundu Lissu.