Kampuni ya Msama Promotions leo imetangaza baadhi ya wasanii wataokuwepo katika Tamasha la Pasaka ambalo limerejea kwa Kishindo.
Tamasha hilo ambalo lilisimama kwa miaka kadhaa linarejea tena Jumapili ya April 2023 ambapo Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama ametaja maboresho yatakayokuwepo katika tamasha hilo.
Pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kama Tumaini Akilimali wa Kenya, Joshua Ngoma wa Rwanda, Upendo Nkone wa Tanzania, Masi Masilia kutokea Congo lakini pia hiyo itakuwa ni siku ya kumuombe Rais wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan ambaye anatimiza miaka miwili katika utawala wake.
“Leo tunaanza sasa kutambulisha waimbaji , tunamuimbaji anatokea Kenya Tumaini Akilimani amekubali kushiriki katika Tamasha la Pasaka”>>> Msama