Habari za Mastaa

Sababu iliyopelekea wazazi wa Linah kumkataa mwanaume aliyempa ujauzito

on

Kupitia XXL ya Clouds FM April 5, 2017 staa wa Bongofleva Linah aliweka wazi kuhusu ujauzito wake kwa namna nyingine baada ya kusema awali wazazi wake walimkataa mpenzi wake aliyempa ujauzito huo kutokana na kuwa dini tofauti.

>>>“Mwanzoni wazazi wangu walimkataa mpenzi wangu kisa ni dini tofauti na mimi, lakini sasa hawana pingamizi. Tumeunganisha damu na kwenye mahusiano naamini upendo, nisingependa mtu anipangie, lakini jambo la wazazi kwa familia za kiafrika ni tofauti.

“Nimebeba ujauzito katika right time kwangu na mwenzangu yupo tayari. Mashabiki wategemee ndoa kabisa muda wowote.” – Linah.

Pamoja na hayo, Linah hakusita kuzungumzia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Mfupi’ ambao ameutambulisha kwenye kipindi hicho, akisema: >>>“Wimbo huu umeandikwa na Mr. Kesho yeye aliona na kusikia kwenye pitapita zake akaona anibless na zawadi ya mashairi haya, na neno Mfupi limetokana na ubunifu wa mtunzi wa wimbo wenyewe kutokana na maneno ya kimo changu.” – Linah.

VIDEO: ‘Sitaki kushindana na watoto, msinishindanishe na Rosa Ree’ Chemical

Soma na hizi

Tupia Comments