Mix

VIDEO: Jeshi la Polisi Makao Makuu wamezungumza kuhusu Polisi waliouawa

on

Baada ya taarifa za kuuawa kwa askari polisi wanane eneo la Kibiti, mkoani Pwani kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika, leo April 14 2017 Jeshi la Polisi Makao Makuu limekutana na wanahabari kutolea ufafanuzi sakata hilo.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani amesema askari waliouawa walikuwa wanatoka kubadilisha lindo ndipo wakashambuliwa kwa risasi katika barabara ya DSM-Lindi na kusema sasa Jeshi hilo linaingia kwenye oparesheni maalum ya kuwatafuta majambazi hao.

 

Soma na hizi

Tupia Comments