Top Stories

Live:Lazaro Nyalandu aibuka mbele ya mkutano wa CCM ,Rais Samia amuita

on

NI Headlines za aliekuwa mwanaharakati wa Chadema, Ndg. Lazaro Nyalandu leo April 30, 2021 ameitwa na Rais Samia mbele ya wanachama wa CCM kuzungumza machache.

Lazaro Nyalandu amezungumza leo hii baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuibuka kuwa Mwenyekiti chama hicho kwa asilimia 100, Kura zilizopigwa ni 1862 na kura zote ni za ndio hakuna kura ya hapana.

‘Mheshimiwa Mwenyekiti ningependa kusema Watanzania wameiona nyota yako wameguswa na kujawa na furaha na matumaini tele kwakuwa Mungu alikuandaa kuwa kiongozi wa Taifa hili tangu misingi ya Ulimwengu’- Lazaro Nyalandu

‘Ni Maombi yetu kwamba mkono  hodari wa Mungu  ukakuongoze katika safari hii iliyotukuka ya kuongoza watanzania wote, uwezo wangu mbele yako na mbele ya Mkutano huu mkuu kielelezo tosha cha wewe kuungwa mkono na watanzania wetu’-Lazaro Nyalandu

Soma na hizi

Tupia Comments