Michezo

Live:Manara anafunguka ukweli wake wa moyoni, Mkataba wa Milioni anajibu

on

Ni Agosti 4, 2021 ambapo aliekuwa msemaji wa Simba SC, Haji Manara anazungumza na Vyombo vya Habari muda huu.Ayo TV iko Mubashara unaweza ukafuatilia tukio hili mwanzo mwisho

“Kama kuna mahali nilifanya makosa haikuwa kwasababu ya Haji bali ilikuwa kwa ajili ya Simba SC sina kitu binafsi na mtu yoyote ila lengo langu ni kuilinda Simba Sport Club“-Haji Manara

“Wakati mwingine nilikuwa nateleza labda nikitete lakini lengo langu ni kuhakikisha Simba Sport Club haisemwi vibaya”- Haji Manara

“Naishukuru sana Serikali hususani kwa Viongozi wote walionipa heshima mimi Haji Manara”- Haji Manara

“TFF hawa ni Taasisi niliofanya nao kazi vizuri sana wakati fulani kweli walinifungia nililipa na nikaitwa katika kamati ya nidhamu nikaeleza kwamba shida yangu sikupewa nafasi ya kusikilizwa haya yote kwaajili ya Simba na niliwahi kupigwa faini ya Milioni 5 kwasababu ya ishu ya Morrison“- Haji Manara

“Haji Manara hana matatizo ila hayo yote kwasababu kuitetea Simba Sport Club”- Haji Manara

Tupia Comments