Ni Agosti 28, 2021 Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa muda huu amekutana na vyombo vya habari anazungumza.
Ayo TV iko live mubashara kutazama kile kinachojiri muda huu.
“Jambo la kwanza ni juu ya maendeleo ya bandari zetu, hali za bandari zetu ni nzuri na zinaendelea kutoa huduma za kusafirisha na kubeba mizigo ndani ya nchi na nje ya nchi kama kawaida licha ya kuwepo kwa changamoto kubwa inayoikumba dunia janga la Covid-19“- Msemaji wa Serikali
“Ningependa kuwapa takwimu kidogo katika miezi sita iliyopita Feb-July bandari zetu zilizopo ukanda wa bahari ya Hindi yaani Tanga, Dar es Salaam na Mtwara na bandari zilizopo katika maziwa yetu yaani Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na zimeongeza idadi ya meli zilihudumia kutoka meli Elfu 1388 ambazo zilihudumia kipindi cha mwaka jana 2020 zimeongezeka hadi kufikia 2206”- Msemaji wa Serikali
“Sasa ongezeko hili kubwa tumelipata zaidi katika bandari ya Dar es Salaam”– Msemaji Mkuu wa Serikali Gerosn Msigwa
MBUNGE JERRY AFUNGUKA SABABU ZA KUTOTOKEA MBELE YA KAMATI JANA