Michezo

Liverpool imekamilisha usajili kwa kumleta Kikosini huyu mchezaji wa sita..

on

Dirisha la usajili wa kipindi cha kiangazi limefunguliwa leo rasmi na klabu ya Liverpool imetangaza kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine baada ya Firmino kuungana na Kikosi hicho wiki iliyopita. 

 Liverpool wamemsaini Nathaniel Clyne kutoka Southampton kwa ada ya uhamisho ya Pound Milioni 12.5, mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka 5.

Nina furaha kutimiza ndoto yangu ya kuja hapa Anfield kuitumikia klabu kubwa kama hii,” Clyne amenukuliwa na mtandao wa Liverpool.

Baada ya Liverpool kuonesha kunihitaji, nilifurahia na nikapenda uhamisho huo ukamilike haraka.“>>> Clyne.

 
Clyne ni staa wa soka ambaye alikuwa amebakiza mwaka mmoja tu kwenye Mkataba wake kuendelea kuichezea Klabu ya Southampton, sasa anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments