Michezo

Kiungo huyu anaweza kuwa mbadala kuvaa viatu vya Steven Gerrard ndani ya Liverpool?

on

Steven GerrardLiverpool imeanza mikakati ya kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya England.

Ikiwa imekata tamaa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu baada ya Chelsea kupewa nafasi kubwa kwa sasa tayari imemwongezea mkataba wa miaka mitano kiungo wao Jordan Henderson mpaka mwaka 2020, baada ya mkataba huo kwa sasa atakuwa akilipwa paundi 100,000 kwa wiki.

son

Jordan Henderson

Henderson alisajiliwa na Liverpool mwaka 2011 kwa paundi milioni 20 akitokea Sunderland baada ya kuonesha kiwango kizuri uwanjani.

Nahodha wa klabu hiyo Steven Gerrard ambaye tayari ametangaza kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu kwenda klabu ya LA Galaxy ya Marekani, imeonekana kama hatoacha pengo lolote kwa kuwa nafasi ya Ucaptain wake itachukuliwa na Henderson.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenyeTwitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter InstaFB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments