Liverpool wanatafuta kumsajili winga wa Brentford Bryan Mbeumo iwapo Mohamed Salah ataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto, linasema gazeti la Daily Express.
Mbeumo, 24, alikuwa na mabao tisa na asisti nane katika mechi 38 za ligi msimu uliopita na alifanikiwa kufunga mabao saba na kutoa asisti tatu katika michezo 15 kabla ya kuumia kifundo cha mguu mwezi Desemba.
Mkataba wa Salah na Liverpool unatarajiwa kuisha mwaka 2025 na klabu hiyo ilikataa ofa ya pauni milioni 150 kutoka kwa klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia msimu uliopita wa joto, jambo ambalo hawana uwezekano wa kufanya tena kama ofa nyingine itawasilishwa.
Liverpool wana orodha fupi ya wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri akiwemo Leroy Sane wa Bayern Munich, Takefusa Kubo wa Real Sociedad na Jarrod Bowen wa West Ham, lakini inaonekana sasa unaweza kumuongeza Mbeumo kwenye orodha hiyo.