Michezo

Matokeo ya mchezo wa Liverpool dhidi ya Norwich haya hapa

on

Screen Shot 2014-04-20 at 3.48.21 PMLiverpool imeendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa uchampion wa ligi kuu ya England baada ya kupata matokeo mazuri dhidi ya Norwich katika mchezo uliomalizika hivi punde.

Liverpool wakiwa ugenini leo wameweza kushinda kwa magoli 3-2 dhidi ya Norwich.
Alikuwa Raheem Sterling aliyeanza kufungua akaunti ya magoli ya Liverpool leo katika dakika ya nne tu ya mchezo, Luis Suarez akaja kuongeza bao la dakika ya 11.

Baaada ya magoli hayo Norwich wakaja juu na kufanikiwa kupata goli kupitia Gary Hooper kwenye dakika ya 54 ya mchezo, ili kujihakikishia ushindi Sterling tena kwenye dakika ya 62 akaifungia Liverpool goli la tatu. Dakika 15 baadae Robert Snodgrass akafunga goli la pili upande wa Norwich.

Norwich walijaribu kutafuta bao la kusawazisha lakini Liverpool walikuwa imara na mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Liverpool wakaibuka na ushindi uliowapeleka kileleni kwa pointi 5 zaidi ya Chelsea anayeshika nafasi ya pili.

Tupia Comments