Club ya Liverpool Leo imeandika historia mpya baada ya kucheza mchezo wao wa nne wa Ligi Kuu England dhidi ya AFC Bournemouth, Liverpool walikuwa nyumbani Anfield na walifanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 9-0.
Magoli ya Liverpool yalifungwa na Luis Diaz aliyefunga mawili dakika ya 3 na 85, Elliot dakika ya 6, Alexander Arnold dakika ya 28, Roberto Firmino aliyefunga mawili dakika ya 31 na 63, Van Dijk dakika ya 45, huku Mephan wa Bournemouth akijifunga na na kuwapa Liverpool goli la saba na Carvaloh dakika ya 80.
Ushindi huo wa kwanza kwa Liverpool msimu huu kwani wamecheza mechi tatu kabla ya Leo na kufungwa moja sare mbili hivyo leo umeamsha morali ya timu lakini kingine ni kuwa Liverpool wameandika historia mpya kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa goli 5-0 kitu ambacho hawajawahi kufanya toka club yao ianzishwe.
Kwa Upande wa Firmino mchezo huo una maana kubwa kwake kwani umemfanya afikishe magoli 100 akiwa na Liverpool toka alipojiunga nao 2015 akitokea 1899 Hoffenheim ya Ujerumani, ushindi wa leo sasa unawafanya Liverpool wawe nafasi ya 9 wakiwa na alama 5.
RAIS WA TFF WALLACE KARIA ATIA NENO “UKISHINDANA NA MAMLAKA UTAUMIA TU, MAWAZO YAKO SUBIRI UWE RAIS”