Michezo

Liverpool yabanwa na vibonde FA Cup

on

Club ya Liverpool ambayo inafanya vizuri kwa sasa katika Ligi Kuu ya England, leo ilikuwa ugenini kucheza dhidi ya Shrewsbury katika mchezo wa Kombe la FA.

Liverpool kutokana na uimara wake EPL na kupata matokeo chanya, wengi waliamini kuwa watapata ushindi dhidi ya Shrewsbury ambao wanacheza madaraja ya chini.

Game inalazimika kwenda kurudiwa Anfield baada ya kufungana 2-2, magoli ya Liverpool yakifungwa na Curtis Jones dakika ya 15 na Donald Love kujifunga dakika ya 46, magoli ya Shrewsbury yote yamefungwa na Jason Cummings dakika ya 65 kwa penati na dakika ya 75.

Soma na hizi

Tupia Comments