Michezo

Liverpool yapata pigo Allison Becker kuwakoss Bournemouth na Atletico

on

Club ya Liverpool ya England ikiwa ina machungu ya kipigo cha kwanza EPL dhidi ya Watford kesho itakuwa nyumbani katika mchezo wa EPL kuikabili FC Bournemouth, lakini Liverpool wataingia wakiwa na wakati mgumu katika mchezo huo kwa sababu imethibitika kuwa wanamkosa golikipa wao namba 1 Allison Becker kutokana na kupata majeraha.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha taarifa hizo jioni ya leo na kuongezea kuwa Becker ataukosa pia mchezo muhimu wa marudiano wa hatua ya 16 bora wa UEFA Champions League dhidi ya Atletico Madrid ambao wanahitaji kupindua matokeo na kutetea Ubingwa wao kutokana na mchezo wa kwanza ugenini Liverpool alifungwa 1-0.

VIDEO: KAULI YA WAZIRI MWAKYEMBE KUHUSU GAME YA SIMBA NA YANGA MARCH 8

Soma na hizi

Tupia Comments