Michezo

Taarifa iliyonifikia kuhusu kocha wa Liverpool Brendan Rodgers…

on

Liverpool imekuwa na wakati mgumu kufuatia kupata matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England.

Taarifa iliyonifikia kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo zinasema kocha wao Brendan Rodgers amefukuzwa kazi baada ya matokeo mabaya ya muda mrefu.

Uamuzi wa kumfuta kazi Rodgers ulifanywa hata kabla ya mchezo ulioisha kwa suluhu dhidi ya Everton ambao uliwaacha Liverpool katika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi ya England.

Meneja wa zamani wa klabu ya Chelsea na Real Madrid Carlo Ancelotti,kocha wa Ajax Frank de Boer na meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund wamehusishwa kujiunga na klabu ya Liverpool katika siku za karibuni baada ya timu hiyo kuuanza msimu kwa kusua sua.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM,TWITTER,FB, YOUTUBE

Tupia Comments