Top Stories

LIVE:Ummy anafunguka mwenendo wa ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri

on

NI WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) MheUmmy Mwalimu ambae muda huu anazungumza na waandishi wa habari  mwenendo wa ukusanyaji wa mapato kwenye kila Halmashauri.

Akizungumza katika mkutano huu  wa waandishi wa habari muda huu  anasema….”Kama ilivyoelezwa jana tulikuwa tutoe taarifa kuhusu ukusanyaji  wa mapato wa Halmshauri pamoja na matumizi yake kwa mwaka wa fedha ambao umemalizi wa mwaka 2020/2021 na Mwaka Fedha kama mnavyofahamu wa Serikali unaanzia tarehe 1 July na kukamilika  tarehe 30 June kwahiyo taarifa ninayotaka kutoa kwa watanzania kupitia kwenu wana habari ni kuanzia 1 July 2020 hadi tarehe 30 June 2021″– Ummy Mwalimu

“Kama mnavyofahamu ofisi ya  Rais TAMISEMI ina utaratibu wa kutoa taarifa za ukusanyaji wa mapato wa ndani ya Halmashauri za Wilaya, Manispaa, na Majiji pamoja na matumizi ya mapato hayo kila robo Mwaka na lengo la hatua hii ni kuongeza uwazi na uajibikaji katika ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri”- Ummy Mwalimu

UNAWEZA UKABONYEZA PLAY KUSIKILIZA KINACHOZUNGUMZWA MUDA HUU NA UMMY MWALIMU 

Soma na hizi

Tupia Comments