NI Agosti 20, 2021 ambapo waziri wa Fedha Dr Mwigulu Nchemba anazungumza na Waandishi wa habari muda huu kuhusu miradi pamoja na Tozo.
“Bilioni 48 na kwaajili ya maeneo ambayo hajawahi kuwa na vituo vya Afya na maeneo ambayo hayajawahi kuwa na Madarasa lakini kwenye Sheria hii tulivyoitunga ilikuwa ni Sheria inatumika pande zote mbili kwahiyo kule Zanzibar ndani ya wiki hizo nne wameweza kukusanyika Bilioni 1.66 ambayo hiyo kwenye shughuli hizo zinazofanana na ya kwetu katika upande wa Muungano”- Nchemba
“Watu wachukue hivyo hivyo hii nchi ni yetu na Pesa iliyokusanywa ni yako na hivi vituo 150 vya Afya vinaokoa maisha ya watu wako hivyo ndivyo ilivyo na Madarasa hayo zaidi ya 500 na Watoto ni wako na utaratibu tuendeshe vipi ni wetu sisi sote”- Nchemba
“KILA MNUNUZI WA UMEME ATAKATWA ELFU 1000 NA KWA NYUMBA YA KAWAIDA ELFU 5000 KWA MWEZI”- TRA