AyoTV

VIDEO: ‘Kwa hiyo watatumika lakini sitawasikiliza’-Rais Magufuli

on

Leo January 11 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kuwataka watanzania kuwapuuza watu wanaoendesha siasa alizozitaja kupitwa na wakati kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Tanzania inakabiliwa na njaa badala ya kuwahamasisha wananchi kufanya kazi.

Rais Magufuli amesema kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwahamisisha wananchi na kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza baa la njaa wakati wanasiasa hao hao ndio waliopitisha Bungeni kutaka nchi iuze chakula.

VIDEO: Agizo la Rais Magufuli kuhusu kufutwa kwa tozo katika zao la kahawa, Bonyeza play hapa chini kutazama 

 

Soma na hizi

Tupia Comments