Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake jijini Dar es slaam, leo November 23 2016 ikiwa ni siku ya tano amefika wilaya ya Ilala na kuzungumza na watendaji mbalimbali wa wilaya hiyo kabla ya kwenda kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Haya ni baadhi ya mambo aliyoyazungumza na watendaji hao wa manispaa ya Ilala
'Tuna idadi kubwa ya watumishi lakini ufanisi ni mdogo, hapa ndio kiini cha ziara yetu'-RC Makonda #DarMPYA #ILALA
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
'Viongozi wetu wa kitaifa wanatukanwa kwa makosa yetu hasa watendaji wa manispaa'-RC Makonda #DarMPYA #ILALA
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
'Watu wa ardhi kazi yenu ni kubadilisha na kuchezesha mafaili matokeo yake mnatuachia migogoro'-RC Makonda #DarMPYA #ILALA
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
'Nimeanzisha utaratibu sisaini nyaraka yoyote ya fidia bila kupita TAKUKURU ili tubaini wezi wa ardhi ya wananchi'- Makonda #DarMPYA #ILALA
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
'Yupo Mtendaji kila unapotajwa mgogoro wa ardhi jina lake lipo, mpaka amegeuka amekuwa kama afisa ardhi'-RC Makonda #DarMPYA #ILALA
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
'Ni heri niwe kiongozi wa siku moja niache alama kuliko kuwa mkuu wa mkoa miaka 20 bila kucha alama yoyote' -RC Makonda #DarMPYA #ILALA
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
'Ziara yetu ni kubaini kama watendaji wanafanya kazi au hawafanyi, nataka tukienda kwa wananchi tuwe na majibu ya kero'-RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
'Katika mkoa wangu idara ninazofikiria kuzifuta ni pamoja na kilimo, wengi wanatulia mshahara tu'-RC Makonda #DarMPYA #ILALA
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
'Tumekuwa na wataalamu ambao wanakula tu mishahara, wengi hawaji na mbinu mbadala'-RC Makonda #DarMPYA #ILALA
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
'Watumishi wanaofanya kazi vizuri mnawaita vihelehele, ni bora niendelee na vihelehele kuliko wapiga majungu na wala rushwa'-RC Makonda
— millardayo (@millardayo) November 23, 2016
VIDEO: ‘Katika watu ambao hamtaingia mbinguni ni watu wa ardhi’-Paul Makonda