Top Stories

Tamko la Magufuli kuhusu usajili mpya wa laini “Watu Milioni 25 wasitumie simu” (+video)

on

Leo April 26, 2019 Rais Magufuli amesema zoezi la kusajili simu kwa njia ya alama za vidole kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa linaloanza May 1, 2019 lianze kwa wale walio na Vitambulisho hivyo, ambao hawana Vitambulisho wapewe muda hadi December.

“Tanzania tuko Milioni 55, vitambulisho vya Taifa vilivyotolewa ni Milioni 13 au 14, unaposema watu wasajili kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa wakati NIDA haijatoa Vitambulisho vya Taifa maana yake unataka Watanzania wasitumie simu” Rais Magufuli

“NIDA bado haijamaliza kutoa vitambulisho unamaanisha Watanzania Milioni 25 wasitumie simu hicho ni kitu ambacho hakiwezekani” Rais Magufuli

“TCRA na NIDA kitu wanachofanya ni kizuri na nchi nyingi duniani wanafanya hivyo ili kuepusha ujambazi na utapeli lakini wafanye hivyo kwa Watanzania Milioni 13 ambao wana Vitambulisho vya Taifa na wale ambao hawana wawape muda hadi December” Rais Magufuli

KWA MARA YA KWANZA MAGUFULI, SUGU KATIKA JUKWAA MOJA MBEYA “NIMEKUSHIKA NA NAKUFUATA”

 

Soma na hizi

Tupia Comments