Duniani

Hii hapa inakuja, safari ndefu zaidi ya Ndege angani kwa saa 19 bila kutua !!

on

Kampuni kubwa ya Ndege Duniani ya Emirates ilitangaza kuanza safari ya Ndege zake kutoka Dubai mpaka Panama ambayo itaanza mwezi February 2016… hiyo ni safari yenye umbali wa Kilometa 13, 820 na iliingia kwenye hesabu kubwa kwa kuwa safari ndefu zaidi ya Ndege Duniani inayochukua mpaka saa 17 na dakika 35, inakuja Rekodi kubwa zaidi !!

Kampuni ya Ndege ya Singapore Airlines iko tayari kuvunja Rekodi hiyo, wao wamejiandaa kuanzisha safari ya Ndege ya umbali zaidi ya Kilometa 15,300.. itachukua mpaka saa 19 angani kutoka Singapore mpaka New York Marekani.

sqfleet2

Singapore wameanza hiyo mipango na wanaamini mpaka mwaka 2018 itakuwa imekamilika na safari zitakuwa zimeanza rasmi, hiyo ikianza itakuwa safari ndefu zaidi ya Ndege angani.. kwa sasa Safari inayoshikilia rekodi ya kuchukua muda mwingi zaidi angani ni ya kutoka Sydney mpaka Dallas Marekani kwa Ndege za Shirika la Qantas Airways.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments