Habari za Mastaa

DIAMOND: “Nafarijika umetabasamu, nitafurahi kusikia wazo la biashara nikuwezeshe”

on

Ifahamu hii kutokea nchini India ambapo muimbaji Hawa hali yake kwa sasa inaendelea vizuri tokea apelekwe nchini humo wiki kadhaa zilizopita kwaajili ya kufanyiwa operation kubwa ya moyo.

Kupitia mtandao wa instagram wa Babu Tale ameelezea kuhusiana na hali ya Hawa na kusema kuwa operesheni ilienda vizuri na sasa yupo karibu kurudi nyumbani Tanzania pamoja na kusema kuwa tumbo lake limepungua tofauti na lilivyokuwa zamani.

Muimbaji Diamond Platnumz ambaye pia ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa kwaajili ya matibabu ya Hawa amefurahishwa na hali yake ya sasa na kutaka kujua ni biashara gani angependea kujihusisha nayo ili amsaidie.

“Nafarijika Kuona Unatabasamu sasa nitafurahi kusikia wazo zuri la biashara toka kwako nikuwezeshe 🙏🏻 #HawaIsSmilingNow

HAMISA MOBETTO AMUONYESHA MPENZI WAKE MPYA MMAREKANI

Soma na hizi

Tupia Comments