Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA, Edward Lowassa alifika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi asubuhi ya leo June 27, 2017 kuitikia wito wa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai ‘DCI’ kwa ajili ya mahojiano ambapo alihojiwa kwa saa 4.
Baada ya kuondoka kituoni hapo, Wakili wa CHADEMA, Peter Kibatala amezungumza na Waandishi wa Habari ambapo alisema:>>>“Alipokea wito wa DCI mahojiano yalihusiana na kile kilichosemakana kuwa kuna kauli alizozitoa ambazo ni za kichochezi, tumefanya mahojiano na polisi wamechukua maelezo yake, ataripoti tena alhamisi saa sita.” – Peter Kibatala.
MAAJABU?!! TUMBO LIMETOBOLEWA LAKINI ANATEMBEA!!!