Top Stories

Lowassa ampongeza Rais Samia kwa hotuba Baraza Kuu UN

on

Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa hotuba yake katika Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kiongozi huyo amefanikiwa kulirejesha taifa katika ramani ya dunia.

Katika Taarifa yake aliyoitoa hivi punde, Lowassa amempongeza na kumshukuru Rais Samia kwa kuifanya vyema kazi ya kuijenga nchi na kisha kuendeleza safari ya kujenga uchumi imara.

“Kupitia hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York Marekani jana Alhamisi, Mama Samia amelirejesha tena taifa letu katika ramani ya dunia,” Lowassa.

LIVE: MAITI KUZUIWA KISA MILIONI 1.6, MUHIMBILI WAFUNGUKA “HATUDAI DENI LA MAITI, TUNADAI MATIBABU”

Soma na hizi

Tupia Comments