Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba, ameandika barua maalumu kwa Jukwaa la Wahariri Tanzania kuonesha kusikitishwa na vurugu zilizotokea katika mkutano wa CUF uliosababisha waandishi kufanyiwa fujo.
Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji wa Azam Two, Prof. Lipumba ameliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo huku akimtaka Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif wakae wazungumze ili wamalize tofauti zao na wakijenge chama:
“Baada ya kulisikia hilo niliamua kuchukua jukumu la kuwaandikia Jukwaa la wahariri barua ambayo ipo mbioni kwenda kwenye ofisi zao kwamba mimi binafsi kama mwenyekiti wa CUF nalaani kitendo cha kupigwa kwa waandishi wa habari na nijambo ambalo hatulikubali kabisa, hatuwezi kujenga Demokrasia ikiwa waandishi wahabari hawafanyi kazi yao katika hali ya amani na utulivu.
“Vile vile kijana wetu amekatwa kisigino kwa panga na anavyo elewa yeye kijana aliyemkata anaitwa Mohamedi Mgonvi na taarifa hii imepelekwa kwenye vyombo vya dola kwaiyo vyombo vya dola inalishughulikia na tulitoa wito ambao ulitolewa na Mkurugenzi wetu wahabari na uwenezi.
“Mimi toka awali nimeeleza kwamba nataka tumalize tofauti za kisiasa kwa mazungumzo tupate suluhu tuheshimu katika ya chama chetu na nimekuwa nikimuita Maalim Seif aje ofisi bugurudi aweze kuzungumza afanye kazi zake kama katibu mkuu na mimi nimemfahamu Maalim Seif mwaka 1973 tukiwa wanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam kwahiyo hatuna sababu ya sisi kuwa na mgogoro huu na kuuruhusu kuendelea.
“Hivi sasa kupitia taarifa zetu zakiuchunguzi zinaonesha kwamba kuna mbinu yakutaka chama hiki kiweze kufutwa kwaiyo kuna matukio ya napangwa njee ya chama ili paweze kutokea vurugu nazikishatokea waseme chama hiki hakifai kuendelea kuwa chama cha siasa na utakuta kuna vyama vingine vya siasa vinashabikia na kutoa wito ilichama hichi kiweze kufutwa.” – Prof. Lipumba.
VIDEO: Waandishi walioshambuliwa kwenye vurugu za CUF wasimulia
VIDEO: Msimamo wa Jukwaa la Wahariri kwa CUF baada ya kushambuliwa wanahabari. Bonyeza play kutazama…