Michezo

Safari ya Samatta England imewadia, hizi ni club 5 za EPL zinamuhitaji

on

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anayeichezea club ya KRC Genk ya Unelgiji, inawezekana ndoto yake ya kucheza Ligi Kuu ya England ikatimia baada ya kuwindwa na timu mbalimbali.

Samatta mwenye umri wa miaka 26 kwa mujibu wa mtandao wa The Sun wa England umeripoti kuwa anawindwa na club tano za EPL na dau la kumng’oa Genk linatajwa kufikia pound milioni 12 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 34.9.

Club ambazo zimeripotiwa kumuhitaji Samatta ni zinazoshiriki EPL ni Watford, Leicester City, Burnley, Aston Villa waliopanda daraja na Brighton wanaopewa nafasi kubwa kumnasa.

Soma na hizi

Tupia Comments