Taasisi ya kuzuia na kupamabana na rushwa inawashikilia watu watatu ikiwemo Gerald Thomas Afisa Mikopo wa Chama cha Waalimu cha Kuweka na Kukopa kwa makosa 282 huku wengine wawili wakikabiliwa na mashtaka 142 kila mmoja.
Kamanda wa Takukuru Kilimanjaro Holle Makungu amesema mashtaka hayo yanayowakabili yanahusu ubadhilifu wa fedha za ushirika huo nakughushi nyaraka za fedha.
Waliotajwa ni Peter Ndelianarua aliyekuwa Mhasibu wa chama hicho pamoja na Rehema Lucas aliyekuwa Karani wa Fedha ambapo watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kesho.
Ulipitwa na hii? BREAKING: TAKUKURU inamtafuta huyu Mtanzania mwenye pesa na mali nyingi
BREAKING: TAKUKURU wanamsaka Biatus Malima Mhadhiri wa Chuo Kikuu