Mix

Kamati ya Bunge ya Mambo ya Ndani wameyapendekeza haya kuhusu sakata la Lugumi

on

May 16 2016 Sakata la Mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises lilitarajiwa kujadiliwa bungeni wakati wa mjadala wa Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Kamati ya Bunge Wizara ya Mambo ya Ndani imependekeza suala la Mkataba huo unaohusisha ufungwaji mashine za alama za vidole ‘fingerprint’ usijadiliwe bungeni na badala yake liachwe kwa kamati ya bunge ya PAC iliyoanza kulifuatilia suala hilo lililoibuliwa na CAG katika ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka 2014/15.

Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani 2016/17 umeahirishwa hadi saa kumi kamili ili kutoa nafasi kwa Kambi rasmi ya upinzani kukutana na kamati ya kanuni ili kuipitia upya hotuba ya kambi hiyo iliyotarajiwa kuwasilishwa kwenye kikao cha asubuhi leo hii.

ULIKOSA UJUMBE WA ZITTO KABWE KWA WAZIRI NAPE? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE 

Soma na hizi

Tupia Comments