Michezo

Luis Suarez karudi Liverpool leo

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay ambaye anaichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Luis Suarez, March 8 ameingia kwenye headlines baada ya mtandao wa sokka.com kuandika na kutoa picha za staa huyo akiwa Liverpool.

Suarez amerejea leo Liverpool kuwatembelea na kuwasalimia rafiki zake katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo Melwood, Suarez amecheza ndani ya klabu hiyo kwa zaidi ya miaka miwili, kabla ya mwaka 2014 kuamua kujiunga na klabu ya FC Barcelona ambayo anaichezea hadi sasa.

the-Uruguayan-striker

Kama utakuwa unakumbuka vizuri, Luis Suarez aliwahi kuichezea klabu ya Liverpool kuanzia mwaka 2011 baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi ambayo alidumu nayo kwa miaka minne, lakini mwaka 2014 ndio akajiunga na FC Barcelona.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andikaAYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFB YOUTUBE

Tupia Comments