Mshambulizi wa Chelsea Romelu Lukaku yuko kwenye rada za Fenerbahce na vile vile vilabu vya Saudi Arabia, linaripoti Gazzetta dello Sport.
The Blues bado wana nia ya kuachana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 na wanaaminika kutafuta ofa yenye thamani ya €43m.
Lukaku alifunga mabao 13 katika mechi 32 za Serie A akiwa na Roma msimu uliopita, na inaripotiwa kwamba anaweza kusalia Italia, huku meneja wa Napoli Antonio Conte pia akimfuatilia.
Lakini kuungana tena na kocha wa zamani wa Man United na Chelsea Jose Mourinho huko Fenerbahce pia kunaweza kuwa kwenye kadi.