Michezo

Luke Shaw na Van Gaal wamekatisha mpango wa beki huyu wa Man United kuhamia Monaco.

on

Beki wa kimataifa wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Marcos Rojo amesitisha mpango wake wa kwenda katika klabu ya Monaco baada ya kukaa na kufanya mazungumzo ya kina na kocha wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal.

Marcos Rojo ambaye alilazimika kukosa mechi za maandalizi ya msimu Marekani ambapo timu ya Man United iliweka kambi, alikosa kambi hiyo kutokana na matatizo ya passport, Marcos Rojo alikuwa katika mipango ya Monaco kama sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa Anthony Martial kujiunga Man United.

Shaw2

Luke Shaw katika mechi aliyovunjika mguu

Mpango wa Marcos Rojo kwenda Monaco ulisimama baada ya wakala mwenye ushawishi katika soka Jorge Mendes kuingilia kati mazungumzo ya David de Gea na Man United kuhusu suala la kuongeza mkataba mpya, lakini kwa upande wa pili Van Gaal alimthibitishia Marcos Rojo asihame klabu hiyo kwani bado yupo katika mipango yake.

Marcos Rojo ambaye anauwezo wa kucheza beki ya kati na ya kushoto kwa umahiri mkubwa anatajwa kuchukua nafasi ya Luke Shaw ambaye alivunjika mguu wiki iliyopita katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya klabu ya PSV Eindhoven.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments