Top Stories

Lukuvi atoa onyo kwa Wakurugenzi “Ni marufuku kutamani lazima umlipe fidia” (+video)

on

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka Maafisa Mipango Miji nchini kuzisaidia wilaya kuhakikisha maeneo yote ya Vijiji yanayochipukia kuwa Miji anapelekewa ili ayatangaze kuwa maeneo ya Mipango Miji.

Lukuvi amesema hayo wakati akizindua ofisi ya ardhi mkoa wa Kigoma ikiwa ni mfululizo wa uzinduzi wa ofisi za ardhi katika mikoa mbalimbali nchini. Tayari ofisi za ardhi kwenye mikoa ya Tanga, Arusha, Manyara, Singida, Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Katavi zimezinduliwa.

Amesema, wizara yake kwa sasa ina mpango wa kupima kila kipande cha ardhi nchi nzima sambamba na kuhakikisha maeneo yanapangwa ili kuepuka ujenzi holela.

‘’Maeneo yote ambayo vijiji vinachipukia nileteeni nitangaze kuwa maeneo ya mipango miji  na maafisa mipango miji mzisaidie wilaya katika hili’’ Lukuvi

”KIGOMA KUNAMATAPELI, HATUFANYI KAZI KWA KUJUANA SISI, MSIJISUMBUE” WAZIRI LUKUVI

Soma na hizi

Tupia Comments