Habari za Mastaa

Lupita Nyong’o kwenye Headlines kwa mara nyingine, awa gumzo tuzo za SAG 2015, Marekani

on

pita

Lupita Nyongo ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni bora zaidi Ulimwenguni na safari ameonekana kuwa gumzo kutokana na muonekano wake mpya katika tuzo za filamu za SAG zilizofanyika Los Angeles, Marekani.

Katika tuzo hizo zilizofanyika jana Lupita alikua kivutio kwa watu wengi kutokana na vazi lake refu lililoandaliwa na mwanamitindo Ellie Saab na mwonekano tofauti wa nywele zake ambazo mara nyingi alikua akionekana na nywele fupi.

Muonekano wake mpya ulikua ukizungumziwa na wageni wengi waliofika katika tuzo hizo na kufanya kuendelea kuiwakilisha Afrika vyema Kimataifa.

lupi2

pitaa

Lupita Nyong”o akiwa na Jared Leto katika tuzo hizo

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook

 

Tupia Comments