Habari za Mastaa

Lupita Nyong’o kasema haya kuhusu movie ya ’12 Years A Slave’ na movie nyingine anazozicheza sasa hivi!

on

Mwigizaji wa Hollywood, Marekani, Lupita Nyong’o aliweka headlines kubwa sana Africa na dunia nzima baada ya staa huyo kucheza movie iliyoingiza mamilioni ya faida kwenye movie Industry ya Hollywood, 12 Years A Slave, movie ambayo pia ilimuwezesha Lupita kupata tuzo ya Oscars mwaka 2014 kama Best Supporting Actress.

Nimekutana na interview moja aliyofanya Lupita Nyong’o na ndani yake amezungumzia vitu vingi ikiwemo, ilikuwaje akapata nafasi ya kucheza script ya movie hiyo na kama ana mipango ya kuja kucheza movie itakayopita kiwango chake kwenye 12 Years A Slave?

LUPITA

Kuhusu kupata nafasi ya kucheza script ya movie ya 12 Years A Slave, Lupita Nyong’o alisema…

>>> nilisikia kuhusu auditions za movie hiyo sema sikuwa New York so nikaipotezea, lakini manager wangu D.D Ray alifanikiwa kuipata ile script kwa ajili ya mteja wake mwengine ndipo alipo kutana na “Patsey” character ambaye alihisi nitaweza kumcheza… nikarekodi mkanda ya kwanza ya role hiyo na ikatumwa kwa manager wangu wa New York, baada ya wiki moja nikaitwa New York kwenye auditions za mwisho na baada ya kukaa kwa saa nzima kwenye foleni nikafanikiwa kupita, na wiki mbili baadae nikapigiwa simu kwenda kukutana na producer wa movie ili kuanza rasmi…<<< Lupita Nyong’o.

attends the 14th annual AFI Awards Luncheon at the Four Seasons Hotel Beverly Hills on January 10, 2014 in Beverly Hills, California.

Badaae Lupita akaulizwa kama atakuja kucheza movie itakayovuka kiwago chake kwenye movie ya 12 Years A Slave movie iliyomuwezesha apate tuzo kubwa ya Oscars, msanii huyo kutoka Kenya alikuwa na haya ya kusema…

>>> ” Sijui kama kuna movie nitakayokuja kucheza ikavuka levo ya 12 Years A Slave, sidhani! Movie ya 12 Years A Slave ipo kwenye levo ya juu sana, stori yake iligusa wengi duniani na imenifungulia milango mingi… lakini kuja kucheza movie ya kuzidi kiwango kile haitokuja kutokea kwa sababu experience niliyoipata ni ya kipekee sana, japo nataka kucheza role tofauti za movie na pia kujaribu character tofauti, na ninashukuru kwa sababu sasa hivi nimepata fursa ya kufanya hivyo na kutanaua kipaji changu...” <<< Lupita Nyong’o.

LUPITA2

Ukiacha 12 Years A Slave, movie nyingine zilizochezwa na Lupita Nyong’o ni pamoja na; Star Wars Episode VII – The Force Awakens inayotegemea kuwa sokoni tarehe 15 December 2015 na The Jungle Book inayotegemea kutoka tarehe 07 April 2016.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments