AyoTV

VIDEO: Mbunge Lusinde alivyoongelea Wapinzani kukosoa safari za nje ya nchi za JK na JPM

on

Bado tunazisogelea headlines za Bungeni Dodoma ambapo leo May 31 2016 Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na Kimataifa kupitia kwa Waziri wake Augustine Mahiga imeomba kutengewa jumla ya Shilingi 151,396,775,000.00 kama bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Katika kipindi cha kupokea michango kutoka kwa wabunge nakukutanisha na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde aliyesimama na kusema ‘Tunao upinzani ambao wanachokisema hawakielewi, walichokisema mwaka jana wanakuja kukijibu walichokikataa mwaka juzi mwaka huu wanakikubali

‘Tulikua na Rais Kikwete anasafiri kila siku hawa wapinzani walisimama bungeni kusema anatumia pesa nyingi anasafiri sana, leo tumempata Rais Magufuli anabana matumizi pesa zinaelekezwa kwenye maendeleo hawa wanasimama kupinga, wanataka tufanye nini?’ – Lusinde

Ukitaka kumtazama zaidi Mbunge Lusinde bonyeza play kwenye hii video hapa chini…

ULIIKOSA HII? MGAWANYO WA BILIONI 151 ZA WIZARA YA MAMBO YA NJE ULIVYOSOMWA BUNGENI LEO

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments