Mmoja wa waanzilishi wa genge la kuuza dawa za kulevya la Medellin amerejea Colombia baada ya kutumikia kifungo cha zaidi ya miaka 20 jela nchini Marekani kwa kosa la ulanguzi wa dawa za kulevya.
Fabio Ochoa Vasquez, ambaye sasa ana umri wa miaka 67, alifukuzwa na serikali ya Marekani na kutua Bogota siku ya Jumatatu akiwa mtu huru.
Ochoa alikuwa mmoja wa wanachama waanzilishi wa cartel maarufu na alikuwa luteni mkuu wa mlanguzi maarufu wa dawa za kulevya Pablo Escobar.
Kundi la Medellin lilitawala biashara ya cocaine na kuendesha kampeni ya vurugu dhidi ya jimbo la Colombia kabla ya Escobar kuuawa mwaka 1993.
Ikithibitisha kwamba hatakiwi na mamlaka ya Colombia, ilisema kuwa Ochoa aliachiliwa “kuunganishwa tena na familia yake”.
Huku kukiwa na wingi wa wanahabari katika uwanja wa ndege, Ochoa alilakiwa na jamaa zake na kumkumbatia bintiye.
Mnamo mwaka wa 2001, Ochoa alisafirishwa hadi Marekani baada ya kukamatwa nchini Colombia mwaka 1999 pamoja na watu wengine 30 wanaodaiwa kuwa wasafirishaji haramu.
Tayari alikuwa ametumikia kifungo cha jela nchini Colombia mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa jukumu lake kama mmoja wa wakubwa wa genge la Medellin.
Pamoja na kaka zake, alikuwa mlanguzi mkuu wa kwanza kujisalimisha chini ya mpango uliowalinda wanachama wa cartel dhidi ya kurejeshwa Marekani ikiwa wangekubali makosa madogo nchini Colombia