Stori Kubwa

Kutana na Habari kubwa Tano zilizoruka kwenye TV leo April 30 2017

on

Endapo hukupata time ya kutazama Taarifa ya Habari kupitia TV za Tanzania April 30 2017 millardayo.com inakupatia fursa ya kutazama habari 5 kubwa zilizosomwa kwenye TV za Tanzania.

Habari ya Chanel 10 – Rais Maguli ahudhuria Ibada Moshi ajumuika na waumini wa kanisa katoliki na kanisa la KKT

Rais John Pombe magufuli leo April 30 2017 amehudhuria ibada katika mji wa moshi mjini mkoa wa kilimanjaro na kujumuika na waumini wa kanisa la Katoliki na kanisa la KKT usharika wa moshi mjini, hata hivyo Rais Magufuli amewahimiza wa Tanzania kwa kuendelea kueneza amani nchini kwakuwa ndo msingi na chachu ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Habari ya Clouds TV – TLS Kuzikutanisha Taasisi

Chama cha wanasheria Tanganyika TLS kimeazimia kuzikutanisha tasisi za kitaaluma, mashirika ya dini na wataalamu wa mwaswala ya siasa pamoja na katiba ilikujadili hatima ya mchakato wa katiba mpya inayopendekezwa ambayo inadaiwa kukwama ambapo hayo ameyasema Rais wa chama hicho cha wanasheria Tundu Lissu.

Habari ya Chanel 10 – Makamu wa Rais azindua Mradi wa Billion 29

Serikali imesema haitasita kuwachukulia hatua kali watendaji, watumishi na wataalamu wanao tumia vibaya pesa za miradi mbalimbali kujinufaisha wenyewe huku wananchi wakiendelea kupata shida, Kauli hiyo imetolewa na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Mabama wilaya ya Ubuyi.

Habri ya Clouds TV – Ombi la ACT wazalendo kwa Rais Magufuli

Siku chache Baada ya Rais Magufuli kupokea ripoti ya wanachi walio gushi vyeti, chama cha ACT wazelendo kimemuomba abadili uwamuzi wa kuwasamehe watumishi watakao jiondoa wenyewe kazini kwani kufanya hivyo nikinyume cha sheria.

Habari ya Chanel 10 – ATCL yarejesha safari zake Mtwara, Billioni 10 zatengwa kukarabati uwanja wa ndege

Shirika la ndege ATCL limefufua safari zake za ndege kutoka mkoni Mtwara hadi Dar es Salaam kwa kutumia ndege mpya ya Bombadier zilizonunuliwa na serikali kwa lengo la kufufua shirika hilo, Naibu waziri wa wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amezindua safari hizo huku nauli yake ikiwa ni Tsh Laki moja na elfu themanini kwa mtu mmoja.

 VIDEO: “Hakuna mtu atapata uongozi CCM kama hajapita pale” – Humphrey Polepole

Soma na hizi

Tupia Comments