Mix

PICHA15: Kampuni ya Mercedes Benz itatengeneza magari haya 300 tu!

on

Nafahamu wapo wapenzi wa magari ya kisasa na leo leo nimeipata hii kuhusu kampuni ya kuunda Magari ya Mercedes kutoka Ujerumani imetangaza toleo jipya la gari lake aina ya Mercedes-Maybach S650 Cabriolet ambalo wameliongezea ubora kutoka kwenye Mercedes S-class Cabriolet.

Kwa mujibu wa Kampuni hiyo imesema itatengeneza magari 300 pekee yatakayokuwa na vitu vingi vya kisasa ambavyo hakuna gari kwenye kampuni yao limewahi kuwekewa. 

Bado Mercedes hawajatangaza bei kamili ya mauzo ya gari hiyo S650 Cabriolet kwenye nchi za Marekani na nchi za Ulaya, ingawa inakadiriwa kuwa itakua kati ya Euro 290,000 na zaidi au kufikia $320,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania Milioni 690.

Mercedes-Maybach ina uwezo wa kufunuka juu imeongezewa ubunifu zaidi kutoka kwenye gari nyingine ya kampuni hiyo ambayo ni S65 AMG Cabriolet. Injini ya Mercedes-Maybach S650 ina nguvu ya 621 horsepower turbocharged V-12.

Naambiwa kingine kizuri kutoka kwenye hii garoi ni rangi zilizowekwa exclusive — kuna nyekundu, nyeupe na na blue — pia kua logo kali ya Maybach zilizowekwa sehemu mbalimbali nje na ndani. Mnunuzi wa gai hili atapewa zawadi pia ya mabegi manne yaliyotengenezwa kwa material ya siti.

Pia unapewa cheti cha utambuzi kutokwa Mkurugenzi wa Mercedes duniani, Dieter Zetsche. Mercedes-Maybach hii inatazamiwa kuleta upinzani kwenye magari mengine kama vile Rolls Royce.

Nimekuwekea hapa picha za muonekano wa gari hilo.

all-together-this-car-can-really-move-it-has-a-top-speed-of-250-kilometers-per-hour-155-mph-and-can-accelerate-to-100-kilometers-per-hour-62-mph-in-a-respectable-41-seconds and-the-maybach-logo-will-project-on-the-floor-when-you-enter-it  even-the-drop-top-itself-can-come-with-flowing-lines-as-a-trim-option heres-a-closer-look-at-the-view-from-the-drivers-seat it-also-comes-with-an-engraving-to-remind-owners-how-rare-the-car-is mercedes-added-quite-a-few-luxurious-touches-to-justify-the-cabriolets-price-tag-the-headlights-are-embedded-with-swarovski-crystals mercedes-maybach-cabriolet mercedes-said-the-interior-was-crafted-to-feature-flowing-lines-in-the-seats-to-create-a-unique-yacht-ambience the-car-also-comes-with-a-virtual-drivers-instrument-and-a-display-on-the-center-console the-car-comes-with-20-inch-wheels the-car-is-powered-by-a-60-liter-v12-engine-with-an-output-of-630-hp-and-738-pound-feet-of-torque the-limited-edition-mercedes-maybach-s650-cabriolet-is-a-four-seat-drop-top-convertible-that-will-hit-markets-spring-of-2017 the-s650-cabriolet-also-comes-standard-with-a-matching-travel-luggage-set-made-by-mercedes-called-the-affinity-the-bag-color-will-match-the-cars-interior

but-mercedes-specifically-said-the-yacht-like-elements-in-the-s650-cabriolet-were-inspired-by-its-arrow-460-granturismo-yacht-unveiled-in-september

Mercedes wanaifananisha Gari hiyo S650 Cabriolet na boti ya kisasa iitwayo Arrow 460 Granturismo

VIDEO: Ulipitwa na Gari jipya alilopewa Harmonize na lebel yake ya Wasafi Classic Baby “WCB”

 

Soma na hizi

Tupia Comments