Michezo

Van Gaal amfunika Moyes vibaya – hii ndio rekodi yake dhidi ya timu kubwa

on

louis-van-gaal-vs-david-moyes-1411559067Makocha David Moyes na Louis van Gaal wameendelea kufananishwa kwa utendaji wao katika benchi la ufundi la Old Trafford.

Mwanzoni mwa msimu wakati mholanzi Louis van Gaal alipokuwa na matokeo mabaya – vyombo vya habari vilikuwa vikitoa takwimu mara kwa mara na kumfananisha na kocha aliyefukuzwa Man United – David Moyes. Safari hii zimetolewa takwimu za makocha hao katika kuiongoza Man United katika mechi dhidi ya timu kubwa sita za juu.

LVG amemuacha mbali Moyes – akiwa na ameshinda asilimia 62.5% ya mechi dhidi ya vilabu vya Top 6 huku David Moyes akiwa na rekodi mbaya ya kushinda 8.33% tu ya mechi hizo.

Manchester United walipata taabu mwanzoni mwa msimu lakini hivi karibuni wamekuwa kwenye kiwango kizuri wakizifunga timu Tottenham, Liverpool, Aston Villa na jana wakaipa kipigo cha mbwa mwizi Man City.

David Moyes aliweza kushinda mechi moja tu kati ya 12 alizoiongoza United dhidi ya Vilabu 6 bora kwenye ligi na United wakamaliza ligi wakiwa nafasi ya 7.

United sasa wanashika nafasi ya 3, wakiwa wanaongoza kwa kupata matokeo mazuri dhidi ya timu zote za Top 6 – huku wakiwa wamebakiwa na mechi 2 tu za vilabu vya juu – Chelsea na Arsenal – lakini Van Gaal ameshaiongoza United kushinda mechi 5 kati ya 8 alizocheza.

Screen Shot 2015-04-13 at 12.56.29 PM

LOUIS VAN GAAL VS DAVID MOYES

 

Tupia Comments