Club ya Olympic Lyon ya Ufaransa imeripotiwa kuanza ushindani wa kisheria na chama cha soka cha Ufaransa kufuatia uamuzi wao wa kumaliza msimu 2019/20 na kuitangaza PSG kama Bingwa.
Lyon watapeleka kesi hiyo katika Mahakama za juu za Ufaransa, ukizingatia msimu huo umemalizika na msimamo kutambulika wao wakiwa nafasi ya 7 hivyo wanakosa walau nafasi ya kucheza Europa League.
Ligue 1 na Ligue 2 Ufaransa zilimalizwa April huku Legue 1 ikiwa zimesalia mechi 10 kumalizia msimu kitu ambacho Lyon kinawaumiza na kulalamika kuwa club zitapoteza mapato ya karibia euro milioni 900.
Rais wa club ya Lyon Jean-Michel Aulas ndio anaongoza malalamiko hayo na tayari ameshaongea ma mamlaka husika akipeleka malalmiko yao Mahakamani.