Michezo

Lyon kupinga Mahakamani kumalizwa kwa Ligue 1 2019/20

on

Club ya Olympic Lyon ya Ufaransa imeripotiwa kuanza ushindani wa kisheria na chama cha soka cha Ufaransa kufuatia uamuzi wao wa kumaliza msimu 2019/20 na kuitangaza PSG kama Bingwa.

Lyon watapeleka kesi hiyo katika Mahakama za juu za Ufaransa, ukizingatia msimu huo umemalizika na msimamo kutambulika wao wakiwa nafasi ya 7 hivyo wanakosa walau nafasi ya kucheza Europa League.

Ligue 1 na Ligue 2 Ufaransa zilimalizwa April huku Legue 1 ikiwa zimesalia mechi 10 kumalizia msimu kitu ambacho Lyon kinawaumiza na kulalamika kuwa club zitapoteza mapato ya karibia euro milioni 900.

Rais wa club ya Lyon Jean-Michel Aulas ndio anaongoza malalamiko hayo na tayari ameshaongea ma mamlaka husika akipeleka malalmiko yao Mahakamani.

Soma na hizi

Tupia Comments