Headlines za mkurugenzi mtendaji wa makapuni ya MeTL Mohammed Dewji kutangaza kuinunua klabu ya Simba zinazidi kushika kasi katika mitandao, ila July 29 2016 katika mkutano na waandishi wa habari Dewji aliulizwa kuhusiana na mpango wake wa kuwekeza bilioni 20 Simba, wakati aliachana na vilabu vya African Lyon na Singida United.
“Niliachana na Singida United kwa sababu timu niliidhamini ikapanda Ligi Kuu, baada ya kupanda Ligi Kuu zikaanza siasa tuachie timu yetu mimi nikajiondoa kuhusu African Lyon niliachana nayo kutokana na kwenda uwanjani halafu hakuna mashabiki, raha ya mpira mashabiki”
ALL GOALS: YANGA VS MEDEAMA SC JULY 16 2016, FULL TIME 1-1